Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo NEWS. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo NEWS. Onyesha machapisho yote
Mbaroni kwa kuzuia kidato cha 4 kufanya mtihani
NEWSPOLISI mkoani Dodoma inawashikilia walimu watatu wa shule za sekondari kwa tuhuma ya kuwazuia wanafunzi wa kidato cha nne, kufanya Mtihani wa Taifa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema kwamba walimu hao wa shule za sekondari za Zoissa na Mnyakongo wilayani Kongwa, walikamatwa Novemba Mosi mwaka huu.
Kamanda Mambosasa alisema kwamba, wakati wa mtihani wa somo la Kiingereza, walimu hao walimzuia mwanafunzi Amina Said wa shule ya sekondari Zoissa kwa madai ya kuwa ni mjamzito na kumpeleka kituo cha afya, kupimwa muda wa mtihani, lakini majibu yalionesha hakuwa na ujauzito.
Aidha, mwanafunzi Bahati Ntigonza wa shule ya sekondari Mnyakongo, alizuiliwa kuingia katika chumba cha mtihani kwa kuwa hakuvaa sare ya viatu, hivyo alirudishwa nyumbani kuvaa viatu huku wenzake wakiendelea na mtihani.
Kamanda Mambosasa aliwataja watuhumiwa waliokamatwa kuwa ni Lukonge Mwezo ambaye ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Mnyakongo, Omari Athumani Mkuu wa Shule ya Sekondari Zoissa na Daud Suleimani John aliyekuwa mwalimu wa zamu katika shule ya sekondari Mnyakongo.
Guardiola ilitubidi kubadili mbinu dhidi ya Barcelona
NEWSKocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amekiri kuwa ilimlazimu abadili mbinu dhidi ya Barcelona katika mechi ya Ligi ya Mabingwa siku ya Jumanne usiku.
Guardiola awali alitamka kuwa ataendelea kung’ang’ania falsafa yake ya pasi nyingi kutokea nyuma, lakini mfumo wa kucheza moja kwa moja uliisaidia City kujipatia ushindi wa 3-1 dhidi ya Barcelona.
Hata hivyo, Muhispania huyo alieleza kuwa mfumo huo wa uchezaji uliwawezesha kufanya mashambulizi ya kushtukiza na kuzua mashambulizi ya klabu yake ya zamani.
Guardiola, 45, alinukuliwa na BBC Sport akisema: “Tulichuana vikali na Barcelona, lakini kwa sasa tumefanya katika namna nyingine. Tumecheza zaidi mipira mirefu kwa sababu bado hatujazoea falsafa.”
“Wamekuwa wakicheza mfumo wao kwa miaka 25. Kwetu sisi, ni miezi mitatu au minne tumeanza kutumia falsafa mpya.”
City sasa wapo pointi mbili nyuma ya Barcelona kwenye kundi C.
Watiwa Mbaroni Kwa kuvujisha mtihani FEKI wa kidato cha nne
EDUCATION NEWSWalimu wa Shule ya Sekondari Hasanga, iliyopo wilayani Mbozi mkoani Songwe na wafanyabiashara wawili, wanahojiwa na vyombo vya usalama mkoani Mbeya kwa tuhuma za kuhusika na utengenezaji wa mitihani feki ya kidato cha nne
Watuhumiwa hao, James Kapinga (36) ambaye anadaiwa kufanya kazi Shule ya Sekondari ya Hasanga pia anajitolea kufundisha Shule ya Sekondari ya Wazazi ya Sangu, Baraka Mwazambe (28), mfanyabiashara na mkazi wa Tunduma na mtaalamu wa masuala ya Tehama (IT), Alex Mochi.
Watu hao kwa pamoja inadaiwa walikamatwa juzi usiku baada ya mwanafunzi mmoja ambaye jina lake na la shule vimehifadhiwa kukutwa na mtihani wa somo la Kiingereza na alipobanwa, inadaiwa aliwataja wahusika hao.
“Mwanafunzi huyu ni wa shule nyingine tena si ya Mbeya, alikutwa na mtihani feki wa somo la Kiingereza, alipohojiwa alieleza mtihani huo ulitoka Mbeya na Serikali ilipofuatilia iliwabaini wahusika ambao walikuwa wanasambaza mitihani feki,” kilisema chanzo kimoja cha habari hii.
Akizungumzia sakata hilo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariamu Mtunguja, alikiri ofisi yake kupokea taarifa juu ya uvujaji wa mitihani na walipofuatilia walibaini mitihani hiyo ni feki.
“Mbeya hakuna mitihani iliyovuja kama inavyoelezwa katika mitandao, ukweli ni kwamba suala hilo lilifuatiliwa ilibainika mitihani inayosambazwa si ile iliyochapishwa na Baraza la Mitihani la Taifa, ni feki na baadhi ya wahusika wanahojiwa na vyombo vya dola,” alisema.
Naye Kaimu Ofisa Elimu Mkoa wa Mbeya, Benedict Sandy, alisema hakuna mitihani iliyovuja.
“Mitandao imekuwa ikitoa taarifa za upotoshaji eti mitihani imevuja, mitihani iliyosambaa na kukutwa na baadhi ya wanafunzi tena si wa Mkoa wa Mbeya ni feki na wahusika wanaodaiwa kuisambaza wamekamatwa.
“Nawaomba wanafunzi wazingatie yale waliyofundishwa, mitihani hiyo inakuja kwa lengo baya la kuwapotezea muda wao na mwisho wa siku kuishia kufeli, watu wanaofanya kazi hiyo wapo kimasilahi,” alisema.
Samir Nasri aonyesha hataki kurudi Manchester City, Apiga Bei mjengo wake
NEWS
Nyota wa Man City, Samir Nasri ameamua kuliuza jumbo lake la kifahari la
mjini Ceshire, England kwa kitita cha pauni million 5.7.
Nasri ambaye sasa anakipiga kwa mkopo Sevilla ya Hispania ameamua kuliuza jumbo hilo lenye ukumbi wa disco, bwawa kubwa la kuogelea, stoo kubwa ya mvinyo na kadhalika
Uamuzi huo wa Nasri mwenye umri wa miaka 29 ni dalili ameamua kubaki Hispania na huenda akaishaiwishi Man City imuuze kabisa.
Nasri ambaye sasa anakipiga kwa mkopo Sevilla ya Hispania ameamua kuliuza jumbo hilo lenye ukumbi wa disco, bwawa kubwa la kuogelea, stoo kubwa ya mvinyo na kadhalika
Uamuzi huo wa Nasri mwenye umri wa miaka 29 ni dalili ameamua kubaki Hispania na huenda akaishaiwishi Man City imuuze kabisa.
Bunduki 11 zakamatwa nyumbani kwa mbunge
NEWSKikosi kazi maalumu kilichoundwa na Serikali kupambana na tatizo sugu la ujangili, kimenasa bunduki 11 ambazo zinasadikiwa kutumika kufanya ujangili na kukamata watu wanne zaidi.
Hatua hiyo imekuja baada ya hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kufanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa operesheni ya kukabiliana na ujangili.
Taarifa zilizopatikana jana zimelidokezea gazeti la Mwananchi kuwa bunduki hizo zilikamatwa nyumbani kwa mbunge wa CCM (jina tunalihifadhi) ambaye bado anasakwa na kikosi kazi hicho.
Matukio hayo yamekuja siku chache baada ya Rais John Magufuli kutaja jina la mtu anayeitwa Mpemba kuhusika na ujangili kwa muda mrefu wakati alipotembelea ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii na kushuhudia pembe 50 za ndovu zilizokamatwa na watumishi wa wizara hiyo.
Siku hiyo, Rais aliwaambia watu aliowaita “vijana” waendelee na kazi yao ya kukamata wauaji wa tembo, akiwahakikishia kuwa Serikali ipo na kuwataka wasiogope mtu yeyote yule
Marekani: Viongozi wa Democratic wamkosoa mkuu wa shirika la upelelezi
NEWSIkulu ya Marekani imeingia katika mgogoro ambao umetikisa kampeni za urais, katika hatua za kufunga kampeni hizo.
Rais Obama amesema hamuamini mkurugenzi wa shirika la upelelezi nchini humo, James Comey,na kuwa anajaribu kushawishi matokeo ya uchaguzi huo.
Viongozi wa juu wa Democratic wamemkosoa vikali Bwana Comey baada ya shirika la upelelezi wiki iliyopita kusema kuwa lilikuwa likichunguza iwepo wa barua pepe mpya zilizogunduliwa zaweza kumuhusu Bi Clinton.
Shirika hilo limeongeza kuwa wanachunguza ili kuona iwapo zimejumuisha taarifa za siri.
Mapema uchunguzi wa shirika la upelelezi la Marekani lilisema kuwa watumishi wa barua pepe binafsi ya Bi Clinton walizifuta barua za makosa ya kihalifu za Bi Clinton.
Akiongea mjini Ohio, Bi Clinton amesema kuwa alikuwa na uhakika kwamba shirika hilo la upelelezi lingesema hivyohivyo kwa mara nyingine.
Kiboko Mnyama Mwenye Jasho Jekundu
NEWSKIBOKO ni miongoni mwa mamalia mkubwa wa familia ya Hippopotamidae. Anapatikana zaidi katika bara la Afrika na anasifika kwa kinywa na meno yake makubwa. Pua, macho na masikio ya kiboko yapo juu ya fuvu la kichwa hali inayomuwezesha kuzamisha sehemu kubwa ya mwili wake kwenye maji au matope na kupata ubaridi kujizuia na mwanga mkali wa jua.
Kiboko hawezi kukaa nchi kavu nyakati za mchana kwa sababu ngozi yake inaathiriwa na mwaka wa jua. Wakiwa majini ngozi zao hutoa majimaji mekendu kwa ajili ya kuzuia kuungua na jua. Ingawa majimaji hayo sio jasho wala damu ni maarufu kwa jina la ‘jasho jekundu.’
Wataalamu wanasema majimaji hayo hutoka kwenye ngozi ya kiboko bila rangi yoyote lakini baada ya muda mfupi huwa mekundu na baada ya saa chache huwa ya kijivu. Wataalamu wanasema maji hayo hubadilika rangi kwa sababu yana kemikali aina mbili zinazofahamika ‘hipposudoric acid’ na ‘norhipposudiric acid’ kwa jina la kitaalamu.
Kemikali hizi zina kazi muhimu katika mwili wa kiboko kwa kuwa huzuia ukuaji wa bakteria wanaosababisha magonjwa na kuzuia ngozi ya kiboko dhidi ya athari zinazotokana na mionzi ya jua. Viboko huhesabiwa kama wanyama wakubwa nchi kavu lakini tofauti na wanyama wengine wakubwa , viboko huishi kwenye maji baridi ya mito na maziwa. Unene wao unawaruhusu kuzama na kuogelea kwenye kina cha chini kabisa cha mto au ziwa.
Kiboko anafananishwa na nguruwe kwa sababu ana kwato na mwili wake una mafuta mengi mithili ya nguruwe. Wapo watu wanaomuita nguruwe maji. Hata hivyo mwili wa kiboko hauna manyoya, ana miguu mifupi na umbo kubwa. Kimo cha mabegani kinafikia mita 1.5 na ana urefu wa mita mita 4.5. Ingawa kiboko ni mnene na ana miguu mifupi ana uwezo wa kukimbia mwendo wa kilomita 48 kwa saa moja.
Hata hivyo taarifa za mwendo kasi wa kiboko zinatofautiana kutokana na maeneo kwa kuwa baadhi ya wanasayansi wanasema anakimbia kwa kilomita 29 kwa saa moja hivyo ana mbio za kasi kuliko binadamu. Kiboko ni mnyama mwenye uwezo wa kuishi majini na nchi kavu. Huishi kwenye maji baridi katika mito na maziwa lakini ana uwezo wa kutembea kwenye nchi kavu mbali na maji.
Kiboko anaishi kwa kula majani na inasemekana kuwa ni mnyama mkorofi na huenda anashikilia nafasi ya kwanza miongoni mwa wanyama wasiopatana na binadamu. Wataalamu wanasema watoto wa simba, chui, fisi, tembo, au nyati akikulia katika makazi ya binadamu wanaweza kuishi bila kuleta madhara makubwa lakini kiboko hana huruma anapokutana na binadamu.
Hata hivyo sio rahisi kumpata mtoto wa kiboko na kumuweka katika makazi ya binadamu kwa kuwa kiboko huzalia majini na ana utaratibu wa kulea mtoto kwa miezi minane hadi mwaka mmoja ndipo anaacha kunyonya. Kiboko anashindana na kifaru mweupe katika kugombea nafasi ya pili ya mnyama mzito kwenye nchi kavu baada ya tembo ambaye anashikilia nafasi ya kwanza ya mnyama mkubwa wa nchi kavu ana uzito wa kilogramu 3,000 hadi 7,000 sawa na tani tatu hadi tani saba.
Taarifa za hivi karibuni zinasema kiboko anashikilia nafasi ya tatu ya mnyama wa nchi kavu akiwa na uzito kati ya kilogramu 1,500 na 3,500 sawa wa tani moja na nusu hadi tani nne wakati faru mweupe ana uzito wa tani 1,500 hadi 4,000 sawa na tani moja na nusu hadi tani nne. Hata hivyo baadhi ya wanasayansi wanasema huenda kiboko ana uzito zaidi lakini hajaweza kuthibitishwa kwa sababu umbo lao kubwa inakuwa vigumu kumpima uzito wao wakiwa mwituni wakati wa kula majani.
Sio rahisi kuwawekea kizuizi wala kuwakaribia wakiwa majini kwa kuwa ni hatari. Makadirio mengi ya uzito yanatokana na operesheni za kuwapunguza zilizofanyika mnamo 1960. Wastani wa uzito kwa kiboko dume ni kati ya kilogramu 1500 hadi 1800. Viboko jike ni wadogo kidogo wakiwa na wastani wa uzito wa kilogramu 1300 hadi 1500. Viboko wakubwa dume wanaweza kuwa wakubwa sana mpaka kufikia kilogramu 4,500 jambo linaloashiria kuwa wanaweza kuwa na uzito mkubwa kuliko faru mweupe.
Viboko dume huendelea kukua muda wote wa maisha yao, huku majike hufikia uzito wa juu wakifikia umri wa miaka 25. Kiboko huishi maji
Alikiba, Diamond, Ommy wakutana kwenye kipengele kimoja Tuzo za ASFA 2016
NEWS
Waandaaji wa tuzo za mitindo za Uganda, Abryanz Style and Fashion Awards
wametangaza majina ya mastaa watakaowania vipengele mbalimbali.
Wakali wa muziki wa Afrika mashariki, Diamond, Alikiba, Ommy Dimpoz na
Sauti sol wamekutana kwenye kipengele kimoja cha ‘Most stylish artiste’
Huku Juma Jux, Nedy Music na Idris Sultan wakikutana kwenye ‘Male Most
dressed Celebrity’
Jokate Mwegelo, Wema Sepatu na Wolper Stylish watachuana na Vera Sidika,
Huddah Monroe na Kate Peyton kweney ‘Female Most dressed Celebrity’
Hii ndio orodha kamili ya Nominees,
FASHION DESIGNER OF THE YEAR
Martin Kadinda (Tanzania)
Sheria Ngowi (Tanzania)
Bobbins & Seif (Uganda)
Moise Turahirwa (Rwanda)
Makeke International (Tanzania)
Jamila Vera Swai (Tanzania)
MOST STYLISH ARTISTE
Males
Sauti Sol (Kenya)
Ali Kiba (Tanzania)
Diamond Platnumz (Tanzania)
Ommy Dimpoz (Tanzania)
Females
Vanessa Mdee (Tanzania)
Avril (Kenya)
Vicotria Kimani (Kenya)
Aika Navy kenzo(Tanzania)
BEST DRESSED CELEBRITY
Males
Nick Mutuma(Kenya)
Juma Jux(Tanzania)
Nedy Music(Tanzania)
Idris Sultan(Tanzania)
Georgie Ndirangu(Rwanda)
Jamal Gaddafi(Kenya)
Females
Jokate Mwegelo(Tanzania)
Vera Sidika(Kenya)
Huddah Monroe(Kenya)
Wema Sepatu(Tanzania)
Kate Peyton (Rwanda)
Wolper Stylish(Tanzania)
MOST FASHIONABLE MUSIC VIDEO
Mamacita – Tinie Tempah ft. Wizkid
Colours of Africa – Diamond Platnumz ft. Mafikizolo
Soft Work – Falz the bahd Guy
Vanessa Mdee – Niroge
No Kissing – Patoranking ft. Sakordie
Aje – Ali Kiba
If I start to talk – Tiwa Savage ft. Dr. SID
Tulale Fofofo – Micasa FT. Sauti Sol
Kontrol – Maleek Berry.
MOST STYLISH COUPLE
Barbie and Bobi Wine (Uganda)
Bonang Matheba & AKA (South Africa)
Annabel Onyango and Marek Fuchs (Kenya)
Zari Tlale and Diamond Platnumz(Tanzania)
Mr & Mrs Ayo Makun(Nigeria)
Elikem and Pokello(Zimbabwe)
CROSSING BOARDERS WITH FASHION
Jidenna
Ugo Mozie
Lupita Nyongo
LOLU ESQ
BEST DRESSED MEDIA PERSONALITY/ENTERTAINERS OF THE YEAR(AFRICA)
Males
Uti Nwachukwu
Falz the bahd Guy
Idris Sultan
Friday James
Ebuka Obi
Derenel Edun
Georgie Ndirangu(Rwanda)
Females
Vimbai Mutinhri
Toke Makinwa
Stephanie Coker
Bolanle Olukanni
Berla Mundi
Bonang Matheba(SouthAfrica)
Tracy Wanjiru(Kenya)
News: Bondia Thomas Mashali auwawa, mwili wake waokotwa vichakani Dar
NEWS
Bondia maarufu wa ngumi za kulipwa nchini, Thomas Mashali, hatunaye.Taarifa zinaeleza ameuwawa kwa kupigwa risasi na mwili wake kuokotwa
vichakani maeneo ya Kimara jijini Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo.
Yassin Abdallah maarufu kama Ustaadhi, mmoja wa viongozi wakongwe wa
mchezo wa ngumi amethibitisha na kusema mwili wa Mashali upo kwenye
chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili
jijini Dar es Salaam.
"Tumethibitishiwa hizo taarifa za majonzi kabisa, mwili upo Muhimbili na msiba upo kwao Tandale," alisema Ustaadhi.
Apple yaongeza bei ya laptopu na kompyuta zake
NEWS
Kampuni ya teknolojia ya Apple imeongeza bei ya laptopu na kompyuta zake nchini Uingereza kwa pauni 100.
Siku ya Alhamisi ,kampuni hiyo ilizindua laptopu za Macbook Pro zikiwa na bei sawa na ile ya Marekani.Lakini kampuni hiyo pia iliongeza bei ya tarakilishi zake ,ikiwemo ile ya Mac Pro ilio na miaka mitatu kwa pauni 100.
Mchanganuzi mmoja alisema kuwa wateja wanafaa kutarajia kuongezwa kwa bei hizo zaidi.
Mike Pence: Democratic iliteua mgombea mwenye mashaka
NEWS
Mgombea mwenza wa Donald Trump, Mike
Pence amesema kuwa tangazo la shirika la kijasusi la Marekani FBI
kuhusiana na kashfa mpya za barua pepe zinazomhusisha Bi Hillary
Clinton, ni wazi kwamba chama hicho kiliteua mgombea mwenye mashaka.
Amesema
hayo huku ikiwa imesalia takriban wiki moja kabla ya kufanyika kwa
uchaguzi mkuu nchini Marekani, ushindani mkubwa ukiwa kati ya Bi
Clinton wa chama Democratic na Bw Trump wa Republican.Meneja wa kampeni wa Bi Clinton John Podesta, hata hivyo ameliambia shirika la habari la CNN kwamba mkurugenzi mkuu wa FBI James Comey, anapaswa kutoa ufafanuzi kuhusiana na hatua yake ya kutoa tangazo tata siku chache kuelekea uchaguzi.
Kwa upande wake Mike Pence amesisitiza kuwa sakata la email dhidi ya Bi Clinton tangu mwanzo imekuwa ni faida katika kampeni zao na zimewasogeza mbele.
Naye mgombea mwenza wa Bi Clinton pia Tim Kaine, amebeza tangazo hilo la FBI na kusema halina maana yoyote.
Tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu nchini Marekani, kumekuwa na tambo nyingi kati ya wagombea hawa wawili ambapo, uamuzi kamili ni katika sanduku la kura hapo Novemba 8 mwaka huu.
Galatasaray kuingia katika mbio za kumnasa Depay
NEWSKwa mujibu wa 'Mirror', klabu ya Kituruki inataka kumsajili Depay na wako tayari kufanya jitihada kwa ajili yake. Lakini ni chaguo moja kwa Depay mwenye umri wa miaka 22.
Depay alijiunga na United mwaka 2015 kutoka PSV Eindhoven na matumaini ya kuanza kazi kubwa katika Ligi Kuu lakini Mourinho hajawahi kumpa wakati wa kutosha kucheza . Depay amekuwa akihusishwa na klabu mbalimbali na timu kama Milan na Juventus wanataka kujiunga nae.
Galatasaray ndio wapo karibu katika kunasa saini yake. Mholanzi huyo anataka kuihama klabu ya Manchester United, ikiwa yeye alicheza msimu huu si zaidi ya dakika kumi.
Mshindi wa Miss Tanzania(Diana) awajibu wote wanao mchafua
NEWS
Saa
cahche baada ya kuvishwa taji, kumeibuka upotoshaji mkubwa kutoka kwa
baadhi ya watu wenye nia ovu ya kutaka kuharibu taswira nzima ya Mshindi
wa shindano la Miss Tanzania 2016, aliyevishwa taji hilo jana usiku
ndani ya jiji la Mwanza,taarifa hizo ambazo zimekuwa zikisambazwa katika
mitandao ya kijamii zikieleza upotoshaji wa taarifa mbalimbali za
mlimbwende huyo zikiwemo na elimu yake.
SEHEMU YA TAARIFA ILIYOKUWA IKIPOTOSHWA KATIKA MITANDAO MBALIMBALI YA KIJAMII HII HAPA CHINI;
MISS TANZANIA 2016
JINA:Diana Edward Lukumai
UMRI:Miaka 18
ELIMU:Shahada(degree)
Hii ina maana;
Alianza Chuo akiwa na miaka 15
Alianza Form one akiwa na miaka 9
Ingawa
sio mshabik wa haya mambo napenda nchukue hii nafasi kuwapongeza Wazazi
wote kama wazazi wa Diana ambao watoto wao wameanza shule ya msingi
wakiwa na miaka miwili
HII NDIO TAARIFA SAHIHI YA MSHINDI WA SHINDANO LA MISS TANZANIA 2016,DIANA EDWARD LOY.
Napenda kuujulisha Umma yafuatayo;
1.
Miss Tanzania 2016/2017 aliyeshinda taji jana jijini Mwanza, anaitwa
Diana Edward Loy na siyo Diana Lukumai kama inavyotajwa mitandaoni.
2.
Mlimbwende huyo amemaliza kidato cha nne 2015 Shule ya Sekondari Arusha
Day na si 2011 kama inavyotajwa mitandaoni kwa malengo ovu.
3.
Diana hajawahi kujiunga na Elimu ya Chuo Kikuu chochote Tanzania au
duniani bali anatarajia kujiunga mwaka huu katika chuo cha IFM kusomea
masula ya kodi ngazi ya stashahada (cheti) ingawa kulingana na ratiba
zake na majukumu yake mapya ikiwemo kushiriki Miss world mapya huenda
akaahirisha mwaka wake wa masomo.
4.
Tunawasihi watanzania kutumia vyema mitandao ya kijamii na si kufanya
"Character assassination" lakini pia tunaheshimu haki yao ya msingi ya
kuhoji masuala ya msingi kabisa kuhusu mtu ambaye ni Public figure na
ataliwakilisha taifa katika anga za kimataifa.
UVCCM ‘kumchongea’ Ndalichako kwa Magufuli
NEWSDakika chache baada ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) taifa, kutoa tangazo la kuwataka wanafunzi waliokosa mikopo wakati wana vigezo, kuandikisha majina yao kupitia barua pepe ya UVCCM, jumuiya hiyo imeahidi kupeleka orodha hiyo kwa Rais John Magufuli
Tangazo la UVCCM limesema vielelezo vya kuthibitisha sifa za mwanafunzi kupata mkopo ikiwemo vyeti vya kifo au vifo vya wazazi au hali ya familia anayotoka, vitumwe kupitia barua pepe ya jumuiya hiyo ambayo ni uvccm1978@gmail.com huku mwisho wa kutuma ni tarehe 4 Novemba 2016.
Akizungumza na MwanaHALISI Online kwa njia ya simu Sylvester Yaredi, Kaimu Katibu Idara ya Uhamasishaji, Sera, Utafiti na Mawasiliano UVCCM, ametoa ufafanuzi wa tangazo hilo ambapo amesema watapeleka orodha ya majina hayo kwa rais kwani wanaamini ataingilia kati suala hilo.
“Hatutachukua fedha kutoka kwenye mfuko wa UVCCM ili kuwasomesha vijana waliokosa mikopo kama baadhi wanavyodhani, tutachofanya ni kuandaa orodha ya wanafunzi pamoja na vielelezo vinavyothibitisha sifa zao kupata mikopo.
Baada ya hapo tutapeleka documents (nyaraka) hizo kwa Rais Magufuli kwasababu yeye amekuwa akifuatilia suala hili kwa umakini, ndiyo maana amekuwa mkali mara kwa mara kwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu pale inapochelewesha malipo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu,” amesema Yaredi.
Kuipeleka orodha hiyo kwa Rais Magufu huenda ikawa ni kumuweka kikaangoni Prof. Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia kwani ndiye msimamizi wa uwajibikaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu (HESLB).
Kwa kipindi cha wiki tatu sasa tangu vyuo vikuu hapa nchini vilipoanza kufunguliwa, vilio vya wanafunzi kukosa mikopo vimesikika vyuoni. Serikali imekuwa ikilaumiwa kwa kupunguza idadi ya wanafunzi wanaonufaika na mikopo.
Vigezo vipya vya kupata mikopo vilivyotangazwa na serikali tarehe 12 Oktoba mwaka huu kupitia kwa Mhandisi Stela Manyanya, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ‘vimefinya’ wigo wa wanufaikaji. Hata hivyo, bado baadhi ya wale wenye vigezo tajwa wamekosa mikopo hiyo.
Wiki mbili zilizopita, Abdulrazaq Badru, Mkurugenzi wa HESLB aliwaeleza wanahabari kuwa kati ya wanafunzi 88,000 walioomba mkopo mwaka huu, watakaopewa ni 21,500 tu. Siku nne baadaye Prof. Ndalichako alinukuliwa akisema, serikali itatoa mikopo kwa wanafunzi 25,000.
Idadi hiyo ni pungufu ya zaidi ya wanafunzi 15,000 ya waliopata mikopo mwaka jana ambapo jumla ya wanafunzi 40,836 walipata mikopo.
Kama hilo halitoshi, mchana wa leo Jumapili ya tarehe 30 Oktoba, 2016 Badru amewaeleza tena wanahabari kuwa, HESLB itawapitia upya wanafunzi wanaoendelea na masomo vyuoni ili kubaini ambao hawakidhi vigezo vipya na kuwaondoa.
Samatta Atokea Benchi Genk Ikiua 2-1 Ubelgiji
NEWSMSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amecheza benchi timu yake, KRC Genk ikishinda 2-1 dhidi ya Westerlo katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji, Uwanja wa Laminus Arena.
Kiungo Mspaniola, Alejandro Pozuelo aliifungia bao la kwanza Genk dakika ya 54 kabla ya mshambuliaji Mgiriki, Nikolaos Karelis kufunga la pili dakika ya 66, wote wakimalizia pasi za mshambuliaji Mjamaica, Leon Bailey.
Na ni Nikolaos Karelis aliyempisha Samatta, Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' dakika ya 66 mara tu baada ya kufunga bao la pili. Bao pekee la wageni lilifungwa na kiungo Mbelgiji, Jamo Molenberghs dakika ya 82.
Huo unakuwa mchezo wa 31 kwa Samatta tangu amejiunga na Genk Januari mwaka huu kutoka TP Mazembe ya DRC, 18 msimu uliopita na 12 msimu huu, akifunga mabao nane, matatu msimu huu na matano msimu uliopita.
Katika mechi hizo, ni 16 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na tano msimu huu, wakati 14 alitokea benchi nane msimu uliopita na 11 msimu huu – na mechi tisa hakumaliza akitolewa, sita msimu uliopita na tatu msimu huu.
Cassper Nyovest aweka historia tena, aujaza uwanja wa Orlando (40k)
NEWS
Cassper Nyovest alithubutu kwa mara nyingine tena na amefanikiwa.
Jumamosi hii, rapper huyo wa Afrika Kusini, aliweka historia kwakuwa
msanii wa kwanza wa nchini humu kuujaza mwenyewe uwanja wa mpira wa
Orlando jijini Johannesburg kwenye show yake aliyoipa jina Fill Up
Orlando Stadium.
Uwanja huo huchukua watu 40,000. Wizkid alikuwepo pia kwa surprise na kuunga na mastaa wengine kumsindikiza rapper huyo.
Closing moment for #FillUpOrlandoStadium !!! Thank you so much!!! Next year we do FNB Stadium!!! New single dropping at 9AM titled #ABASHWE,” ameandika kwenye Instagram.
Uwanja huo huchukua watu 40,000. Wizkid alikuwepo pia kwa surprise na kuunga na mastaa wengine kumsindikiza rapper huyo.
Closing moment for #FillUpOrlandoStadium !!! Thank you so much!!! Next year we do FNB Stadium!!! New single dropping at 9AM titled #ABASHWE,” ameandika kwenye Instagram.
Mechi za ligi daraja la kwanza msimu wa 2016/2017 kuendelea leo
NEWSMechi za Ligi Daraja la Kwanza msimu wa 2016/2017 zitaendelea tena leo Oktoba 29, 2016 kwa michezo minane ya makundi A, B na C.
Katika kundi A kutakuwa na michezo miwili ambako Polisi Dar itacheza na Lipuli ya Iringa kwenye Uwanja wa Karume, ulioko Ilala jijini Dar es Salaam wakati Friends Rangers itasafieri hadi Tanga kupambana na African Sports kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Jumatatu Oktoba 31, mwaka huu kutakuwa pia na michezo miwili ya kundi hilo ambako Mshikamano na Ashanti zitachuana jijini Dar es Salaam kwenye kwenye Uwanja wa Karume, ulioko Ilala jijini.
Kundi B kutakuwa na michezo mitatu kwa siku ya leo Oktoba 29, 2016 ambako Mlale itaikaribisha Coastal Union ya Tanga kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati Kurugenzi ya Mafinga itakuwa mwenyeji wa Kemondo ya Morogoro kwenye Uwanja wa Uwambi huko Iringa ilhali Njombe Mji itacheza na Mbeya Warriors ya Mbeya huko Makambako.
Katika kundi hilo, KMC ya Dar es Salaam itacheza Jumatatu Oktoba 31, mwaka huu kwenye Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani.
Kadhalika Kundi C kutakuwa na mechi tatu. Mechi hizi ni kati ya Singida United itayocheza na Polisi Mara kwenye dimba la Namfua mjini humo wakati kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Polisi itakuwa mwenyeji wa Rhino ya Tabora ilhali Panone ya Kilimanjaro itacheza na Mgambo JKT ya Tanga kwenye Uwanja wa Ushisirika mjini Moshi.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)




















