Bunduki 11 zakamatwa nyumbani kwa mbunge

02:48



Kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Serikali kupambana na tatizo sugu la ujangili, kimenasa bunduki 11 ambazo zinasadikiwa kutumika kufanya ujangili na kukamata watu wanne zaidi.
Hatua hiyo imekuja baada ya hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kufanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa operesheni ya kukabiliana na ujangili.
Taarifa zilizopatikana jana zimelidokezea gazeti la Mwananchi kuwa bunduki hizo zilikamatwa nyumbani kwa mbunge wa CCM (jina tunalihifadhi) ambaye bado anasakwa na kikosi kazi hicho.
Matukio hayo yamekuja siku chache baada ya Rais John Magufuli kutaja jina la mtu anayeitwa Mpemba kuhusika na ujangili kwa muda mrefu wakati alipotembelea ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii na kushuhudia pembe 50 za ndovu zilizokamatwa na watumishi wa wizara hiyo.
Siku hiyo, Rais aliwaambia watu aliowaita “vijana” waendelee na kazi yao ya kukamata wauaji wa tembo, akiwahakikishia kuwa Serikali ipo na kuwataka wasiogope mtu yeyote yule

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »