Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amekiri kuwa ilimlazimu abadili mbinu dhidi ya Barcelona katika mechi ya Ligi ya Mabingwa siku ya Jumanne usiku.
Guardiola awali alitamka kuwa ataendelea kung’ang’ania falsafa yake ya pasi nyingi kutokea nyuma, lakini mfumo wa kucheza moja kwa moja uliisaidia City kujipatia ushindi wa 3-1 dhidi ya Barcelona.
Hata hivyo, Muhispania huyo alieleza kuwa mfumo huo wa uchezaji uliwawezesha kufanya mashambulizi ya kushtukiza na kuzua mashambulizi ya klabu yake ya zamani.
Guardiola, 45, alinukuliwa na BBC Sport akisema: “Tulichuana vikali na Barcelona, lakini kwa sasa tumefanya katika namna nyingine. Tumecheza zaidi mipira mirefu kwa sababu bado hatujazoea falsafa.”
“Wamekuwa wakicheza mfumo wao kwa miaka 25. Kwetu sisi, ni miezi mitatu au minne tumeanza kutumia falsafa mpya.”
City sasa wapo pointi mbili nyuma ya Barcelona kwenye kundi C.
EmoticonEmoticon