Mike Pence: Democratic iliteua mgombea mwenye mashaka

22:57

Mgombea mwenza wa Donald Trump, Mike Pence amesema kuwa tangazo la shirika la kijasusi la Marekani FBI kuhusiana na kashfa mpya za barua pepe zinazomhusisha Bi Hillary Clinton, ni wazi kwamba chama hicho kiliteua mgombea mwenye mashaka.
Amesema hayo huku ikiwa imesalia takriban wiki moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini Marekani, ushindani mkubwa ukiwa kati ya Bi Clinton wa chama Democratic na Bw Trump wa Republican.
Meneja wa kampeni wa Bi Clinton John Podesta, hata hivyo ameliambia shirika la habari la CNN kwamba mkurugenzi mkuu wa FBI James Comey, anapaswa kutoa ufafanuzi kuhusiana na hatua yake ya kutoa tangazo tata siku chache kuelekea uchaguzi.
Kwa upande wake Mike Pence amesisitiza kuwa sakata la email dhidi ya Bi Clinton tangu mwanzo imekuwa ni faida katika kampeni zao na zimewasogeza mbele.
Naye mgombea mwenza wa Bi Clinton pia Tim Kaine, amebeza tangazo hilo la FBI na kusema halina maana yoyote.
Tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu nchini Marekani, kumekuwa na tambo nyingi kati ya wagombea hawa wawili ambapo, uamuzi kamili ni katika sanduku la kura hapo Novemba 8 mwaka huu.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »