‘Nitaifunga tena Simba siku ya Jumamosi – Tegete’

11:40

MSHAMBULIZI, Jerson Tegete anaamini pointi 8 wlizofanikiwa kukusanya katika michezo minne ya mwisho katika ligi kuu Tanzania Bara zitaibeba timu yake ya Mwadui FC katika game vs Simba SC mwishoni mwa wiki hii katika uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Mwadui FC ilikuwa katika wakati mgumu hadi kufikia hatua ya kujiuzulu kazi kwa kocha Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’.

Walishinda 2-0 nyumbani vs African Lyon, wakaenda Pwani na kulazimisha sare ya kufungana 1-1 dhidi ya JKT Ruvu, kisha sare kama hiyo vs Ruvu Shooting na wakaichapa 2-1 timu ya Ndanda FC katika uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.

“Mechi yetu ijayo itakuwa ni ya kawaida tu, sema ngumu kwa jina la Simba lakini uwanjani itakuwa rahisi na tunajiandaa vizuri.” anasema Tegete mshambulizi wa Mwadui FC.

Mwadui imefanikiwa kufunga magoli 9 tu katika game 11 walizokwisha kucheza, wanaivaa Simba ikiwa imeruhusu magoli matatu tu.

“Lolote linaweza kutokea, tulikuwa katika kipindi kigumu lakini sasa timu imeanza kukaa sawa kama umeona mechi zetu nne za mwisho tumedroo mbili na tumeshinda mbili, mechi ya tano ni dhidi ya Simba siku ya Jumamosi kitu chochote kinaweza kutokea.” anasema Tegete mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC ambaye ni kati ya wachezaji watatu waliopata kufunga magoli mengi katika historia ya pambano la Yanga v Simba Tegete aliifunga Simba mara tano akiwa mchezaji wa Yanga.

“Tangu nimeondoka Yanga nimecheza dhidi ya Simba mara moja tu katika mechi ya msimu uliopita katika uwanja wa Kambarage lakini sikufanikiwa kufunga, Jumamosi naweza kufunga inshallah.”

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »