September 10 2016 ilikuwa siku ya
kihistoria kwa makocha waliokuwa na upinzani tokea wakiwa katika Ligi
Kuu Hispania Jose Mourinho na Pep Guardiola, wakati huo walikuwa
wanakutana kwa mara ya kwanza wakiwa wanafundisha vilabu pinzani vya
Ligi Kuu England Man United na Man City.
Siku hiyo ikiwa ndio ya kwanza kukutana
kwa Mourinho na Guardiola wakiwa katika Ligi Kuu England, ulimwengu
ulishuhudia Man United ya Jose Mourinho ikifungwa na Man City ya Pep
Guardiola kwa magoli 2-1, magoli yaliofungwa na Kelvin De Bruyne dakika
ya 15 na Kelechi Iheanacho.
Sasa usiku wa October 26 wapinzani hao wakakutana tena katika mchezo wa
EFL Cup wakiwa katika dimba la Old Trafford, Man United ilifanikiwa
kuifunga Man City kwa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na Juan Mata
dakika ya 54 na kuufanya mchezo umalizike kwa Jose Mourinho kulipa
kisasi cha September 10 2016.
EmoticonEmoticon