Jumanne hii katika mitandao ya kijamii kulikuwa na majibizano kati ya mashabiki wa Diamond na AliKiba baada ya Diamond Platnumz kupost kipande cha video kikionyesha nyumba yake ya Afrika Kusini huku akizungumza maneno ambayo yameonyesha kuwakasirisha baadhi ya watu.
Mzozo huo katika mitandao ya kijamii ulikuwa zaidi baada ya H Baba
ambaye pia aliwahi kutofautiana na Diamond Platinumz siku za nyuma kutoa
maoni yake katika video hiyo ya Diamond huku akionyesha kutoridhishwa
na kitendo alichofanya Diamond.
H Baba kupitia kipindi cha U-Heard cha Clouds FM, alimtaka Diamond
kuonyesha documents za makabidhiano ya nyimbo hiyo na siyo kuonyesha
picha katika mitandao ya kijamii.“Siku zote mimi ninachojua mtu anayependa kuwatangazia watu ni mstaarabu sana na kitu cha kwanza mtu anaponunua nyumba lazima apewe mkataba then angepiga picha akiwa anasaini siyo wanatupostia picha tu. Anapost picha kwasababu Alikiba amepost nyumba na yeye ndio apost? Unatakiwa kumpongeza tu muziki ni ushindani sio kujibizana kwa picha,”
Hata hivyo Team Kiba walipost picha ya nyumba ambayo walidai ni ya AliKiba lakini muimbaji huyo wa wimbo ‘Aje’aliikana nyumba hiyo huku akidai hana tabia ya kuonyesha vitu vyake katika mitandao ya kijamii.
Hatua hiyo ilimfanya Diamond arudi tena kupitia instagram yake na kuandika:
"Asa kunya nakunya mie makalio yanawauma wengine, eti inahuu….? Wambie wasininunie mie, wakazane….halaf hii clip naomba wanangu mnisaidie kuwatag wote waliokuwa busy kupost na kuzungumza Kuwa nyumba hii si yangu….waambie hizi ndio kwanza rasharasha clip hata kupost sijaanza bado….soon naamia ndani…halaf nlisahau, wakikwambia mie mswahili wambie Mswahili haswaaa… halaf uswahili wangu najua kuutumia na umefanya leo niwe na kibanda south asa wao Uzungu wao Umewapa nini
EmoticonEmoticon