Ujumbe maalumu kwa wanafunzi wa kidato cha nne wanaotaraji kuanza mtihani wa taifa

11:48

Kama tujuavyo ya kwamba zimebaki siku chache ambapo vijana zetu, ndugu, rafiki,watoto wetu wa kidato cha nne waanze mitihani yao ya kihitimu elimu ya sekondary "o-level". Inawezekana labda hii taarifa ikawa ni ngeni kwako ili nitumie kalamu yangu kukumbusha ya kwamba kuamzia tarehe 1.11.2016, ndiyo siku ambayo mitihani hiyo itaanza.

Yafutayo ni mambo ya msingi ya kuyafahamu kabla ya kuanza mtihani Wa taifa;

Zingatio; Mtangulize mwenyezi Mungu kwanza kila wakati.

1. Tuliza akili yako na ondokana na hofu.
Inawezekana hapo awali ulikuwa na mambo mengi sana, ambayo kimsingi hayana mchango wowote katika safari yako ya masomo. Kama ndivyo hivyo nakusihi achana na mambo hayo kwani endapo utaendelea nayo yatakuwa ni kikwazo kikubwa sana katika mitihani yako.

Pia katika suala hili ni vyema ukaatumia nguvu kidogo katika kujikumbusha mambo ambayo naaamini ya kwamba ulikwisha kusoma hapo awali. Pia inawezekana zipo maada ambazo hakuzisoma kabisa, hivyo muda huu ambao umebaki ni muda kidogo ambapo kama utatumia muda huu kusoma maada hizo (topics) utajikuta umechanganyikiwa zaidi. Hivyo wito wangu kwako ni kwamba ni vyema ukatumia muda huu kuweza kupitia kusoma zile maada ambazo ni vyema ulikuwa unazifahamu.

Jambo jingine la msingi ni kwamba ni vyema siku za mitihani ukawahi kulala, ili uwahi kuwahi kuamka mapema ili kufanya maandalizi ya awali kabla ya mtihani, mfano kuandaa kalamu za kuandikia, rula pamoja ni vitu vingine vya msingi ambavyo vitatakiwa katika chumba cha mtihani.

Lakini hata hivyo katika masula ya afya nikumbushe ya kwamba inawezekana vipo baadhi ya vyakula ukila huwa vinakuathiri kwa namna moja ama nyingine, kama ndivyo hivyo usivitumie vyakula hivyo kipindi chote cha mitihani yako. Kwani ukifanya hivyo utaweza kuugua na kutoweza vizuri mitihani yako.

Wahi kufika katika eneo la kufanya mtihani.
Kitaalumu ni kwamba  kufanya hivi huongeza uwezo wa kujiamini. Unashauriwa ya kwamba ufike eneo la kufanyia mtihani angalau nusu saa kabla ya mtihani kuanza ili uweza kuyazoea mazingira.

NB; wazazi kama mwanao anaishi naye nyumbani, katika wiki zile za mitihani epuka sana kumpa kazi ngumu mwanao ambazo zitamfanya ashindwe kutuliza akili yake hatimaye kuweza kushindwa kujiandaa vizuri.

Mambo ya msingi ya kuzingatia katika eneo la mtihani.
1. Soma maelekezo vizuri ya namna ambavyo unatakiwa kufanya mtihani husika. Kwani watu wengi hufeli kwa sababu hushindwa kufuata maelekezo ya mtihani husika. Malekezo hayo ya mtihani huandikwa mbele ya mtihani huo soma mara nyingi maelezo hayo kisha uyaelewe.

2. Soma maswali  yote kwa afasaha,
kisha tafuta maswali ambayo unayaweza kuyajibu vizuri kisha uanze kuyajibu. Maswali ambayo unahisi yana utata kwako yafanye yawe ya mwisho. Pia anza na maswali ambayo huwa yana mlolongo mrefu kama vile insha (essay)  kwani endapo utayafanya maswali hayo yawe ya mwisho huenda akili yako ikawa imechoka hivyo ukashindwa kufanya vizuri.

3. Tafuta wazo kuu la swali.
Hii ndio siri kubwa ambayo imejificha kuhusu ufaulu wa mitihani yako, kwa muuliza swali lipo jibu ambalo analitegemea kutoka kwako, kama ndivyo hivyo jaribu kujiohoji kuhusu kiini cha swali kipo wapi? Baada ya kupata kiini hicho ndipo ambapo unatakiwa kutuliza akili yako kisha uanze kujibu na si kukurupuka kujibu kama ambavyo wafanyavyo watu wengi.

4. Zingatia matumizi sahihi ya muda.
Muda ni sehemu ya mtihani, hivyo baada ya kujua unatakiwa kufanya maswali mangapi  unachotakiwa kufanya ni kujua je! kila swali utatumia dakika ngapi kufanya swali hilo? Hilo ni jambo jema zaidi. Usipoteze muda mwingi kwa swali ambalo usilolijua.

5. Pitia majibu yako yote.
Ukishamaliza mtihani wako unachotakiwa kufanya ni kwamba upitie vizuri tena kwa ufasaha majibu ya mtihani wako. Kufanya hivi kutakusaidia kujua kama maswali ambayo ulitakiwa kuyajibu kama umekwisha yajibu. Kama kana mahali pia hukumalizia kujibu ndio wakati mwafaka wa kufanya hivyo.

Kwa imani yeyote ile tumia nafasi hiyo kumshukuru Mungu kabla ya kukusanya mtihani wako.
NB; Kama uliyekuwa unayesoma Makala haya si muhusika wa ufanyaji wa Mitihani hiyo, naomba utumie nafsi hiyo kwa hayo ambayo umeyasoma kuwambusha anagalau hata wanafaunzi hao Wa kidato cha nne mambo hayo.

Nikutakie mtihani mwema, Mwenyezi Mungu akusaidie uweze kufanya vizuri na hatimaye kufaulu vizuri. Amina

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »